Wapigakura wanapiga kura leo Jumanne kwa uchaguzi wa gavana katika majimbo ya Marekani ya Virginia na New Jersey ambayo yanafuatiliwa kwa karibu kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula mwaka ujao.
Katika jimbo la Virginia, Terry McAuliffe ambaye aliwahi kuwa gavana wa jimbo hilo kutoka mwaka 2014 hadi 2018, anakabiliana na m-Republican, Glenn Youngkin aliyeingia katika siasa. Wagombea wote wawili walifanya kampeni zao za mwisho jana Jumatatu, katika vitongoji vya kaskazini mwa Virginia, nje ya mji wa Washington.
Youngkin aliwaambia wafuasi wake hatma ya baadae ya nchi hii itaamuliwa katika kura ya leo wakati McAuliffe alisema dau ni kubwa. McAuliffe anaonekana kushuka katika kura za maoni katika miezi ya karibuni, kama vile viwango vya uongozi wa Rais Joe Biden, m-Democratic vinavyoshuka.
Wakati huo huo Rais wa zamani Marekani, Donald Trump anaunga mkono kampeni za Youngkin ikiwa ni pamoja na kuitisha mkutano wa chama cha Republican hapo Jumatatu usiku.