Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 02:12

Trump anatarajiwa kuendeleza wimbi la ushindi


Mgombea urais wa Republican, Donald Trump akiongea kwenye mkutano wa kampeni huko Wilkes-Barre, PA.

Mgombea kiti cha rais kwa ajili ya chama cha Republikan,Donald Trump, anatarajiwa kushinda kwenye majimbo yote matano yanayofanya uchaguzi wa awali leo Jumanne akitarajiwa kujipatia wajumbe zaidi ili kuweza kuteuliwa kukiwakilisha chama hicho.

Kura za leo zitapigwa kwenye majimbo ya Pennsylvania, Connecticut, Delaware, Maryland na Rhode Island huku wapinzani wawili waliobaki kwenye chama hicho wametangaza mkakati wa kampeni ya pamoja dhidi ya Trump ili kumzuia kupata wajumbe wa kutosha.

Trump amesema kuwa juhudi za seneta wa Texas, Ted Cruz, na gavana wa Ohio, John Kasich, ni kutapatapa.

Kwenye kampeni za chama cha Demokrat, Hillary Clinton anaongoza dhidi ya senator wa Vermont, Bernie Sandrers, kwenye ukusanyaji maoni katika majimbo manne. Sanders akionekana kuongoza katika jimbo la Rhode Island.

XS
SM
MD
LG