Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:00

Democrat yaongeza nguvu California


Mgombea wa urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton.
Mgombea wa urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton.

Wanachama wa chama cha Democratic nchini Marekani wanaongoza kampeni kabambe kuwavutia wapigaji kura wenye asili ya nchi za Amerika Kusini kabla ya uchaguzi wa awali wa jimbo la California utakaofanyika Juni 7.

Raia hao wanaofahamika kama Wahispania ni karibu theluthi moja ya wakazi wa jimbo hilo, na wanashawishiwa na kampeni za wagombea urais wa chama hicho Bi. Hillary Clinton na Seneta Bernie Sanders.

Wakati huo huo wanaojitolea wamekua wakiwaandikisha wapiga kura wapya, kuzunguka mitaani na kuwapigia simu wademokrat waliojianidikisha.

Kwa kiasi fulani wakazi hao wanahamashishwa kushiriki kujaribu kupinga mgombea mtarajiwa wa chama cha Republikan Donald Trump ambaye amesema Mexico inatuma watu wake wabaya ikiwa ni pamoja na wabakaji hapa Marekani kati ya wahamiaji wanaovuka mpaka kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG