Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:09

Wapinzani wa Museveni wakasirishwa na matamshi yake.


Mgombea huru wa Uganda Amama Mbabazi akizungumza na waandishi wa habari.
Mgombea huru wa Uganda Amama Mbabazi akizungumza na waandishi wa habari.

Wapinzani wa rais Yoweri Museveni wa Uganda wamekerwa na matamshi aliyoyatoa rais huyo hivi karibuni akiashiria kwamba hawezi kuondoka madarakani hata kama akishindwa kwenye uchaguzi mkuu unaoytarajiwa kufanyika mwezi ujao.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:38 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika mkutano aliofanyia wilayani Ntungamo mwishoni mwa wiki iliyopita alijilinganisha na mkulima wa ndizi asiyeweza kuacha mazao yake kuvunwa na mtu mwingine, matamshi hayo yamewakera vigogo wa upinzani wakionya kwamba endapo Museveni anamaanisha hivyo , basi ataitumbukiza Uganda katika matatizo.

Naye mgombea huru Amama Mbabazi amekionya chama tawala NRM dhidi ya wizi wa kura kwa kung’ag’ania kubakia madarakani amelinganisha wizi huo wa kura na mapinduzi ya kijeshi akiwataka wafuasi wake kulinda kura zao katika vituo vya kupigia kura.

Mbabazi ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika utawala wa Rais Yoweri Museveni amedai wizi wa kura hutekelezwa jijini Kampala kwenye tarakilishi na hilo ni rahisi kwake kudhibiti.

XS
SM
MD
LG