Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:12

Uchaguzi Sudan waongezwa muda


Rais Omar Al Bashir akipiga kura yake mjini Khartoum Sudan, Aprili 13, 2015.
Rais Omar Al Bashir akipiga kura yake mjini Khartoum Sudan, Aprili 13, 2015.

Sudan Jumatano imeongeza muda wakupiga kura kwa siku moja baada ya wapiga kura wachache kujitokeza jambo ambalo upinzani unasema linaashiria wapiga kura kutokuwa na hamasa na uchaguzi huo.

Rais Omar al-Barshir kwa kiasi kikubwa anatarajiwa kushinda. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, AFP, kiongozi huyo mwanajeshi mwenye umri wa miaka 71 na ambaye ameshtakiwa na mahakama ya kitaifa ya uhalifu ICC kwa uhalifu wa vita, anajaribu kuendeleza uongozi wake wa muda wa robo karne bila kupingwa.

Bw Bashir anakabiliana na wapinzani 13 wasiojulikana sana kwenye uchaguzi ambao umesusiwa na vyama vikuu vya upinzani katika nchi yenye idadi ya watu milioni 38. Wawili kati ya wagombea 15 wanaowania kiti cha urais ni Omar Awad al Karim na Ahmed Radhi ambao wamejiondoa kwenye uchaguzi huo baada ya muda wa upigaji kura kuongezwa hapo jana.

XS
SM
MD
LG