Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 07:12

Hali Tete Mogadishu Wakati wa Uchaguzi wa Rais Leo


Wanajeshi wa Somali wakiwa wamejiandaa kuhakikisha usalama katika uchaguzi wa rais leo.
Wanajeshi wa Somali wakiwa wamejiandaa kuhakikisha usalama katika uchaguzi wa rais leo.

Hali ya hatari imeendelea kujitokeza mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia wakati ambapo wabunge wanategemewa kupiga kura kumchagua rais wa Somalia Jumatano.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa kumekuwa na uvunjifu wa amani karibu na uwanja wa ndege ambapo uchaguzi huo unafanyika, na wakazi wa maeneo ya Waberi Kusini Magharibi ya mji mkuu huo wakithibitisha hali hiyo tete.

Hata hivyo ripoti zinaelezea kuwa njia kuu zote zimewekewa vizuizi na uwanja wa ndege haupitiki.

Kwa mujibu wa taarifa za mbalimbali sasa uchaguzi huo utafanyika Uwanja wa ndege wa Mogadishu kwa sababu ya kuhakikisha usalama wa wabunge.

Imeripotiwa kuwa sababu kubwa ya kuhamishwa uchaguzi huo ni kutokana na vitisho vya uvunjifu wa amani na kubainika kuwa rushwa inatembea kabla ya uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG