Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 03:08

Uchaguzi Rwanda watarajiwa kukipa nguvu chama cha RPF


Mwananchi akipiga kura nchini Rwanda.

Wapiga kura nchini Rwanda wanaendelea kushiriki uchaguzi wa bunge Jumatatu, ambapo duru za siasa zinasema unatarajiwa kukipa nguvu chama tawala cha Rwanda Patriotic Front – RPF- kwa kupata wingi wa viti bungeni.

Uchaguzi huo ambao ulianza siku ya jumapili kwa wapiga kura walioko nje ya nchi, unaendeshwa katika vituo vya kupigia kura 2,500.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika anaripoti kuwa zaidi ya wapiga kura milioni saba waliosajiliwa watawachagua wabunge 80, huku viti 24 kati ya hivyo vikitengwa kwa ajii ya wanawake, viwili kwa ajili ya vijana, na kimoja kwa ajili ya walemavu.

Kadhalika zaidi ya wagombea 500 kutoka vyama vitano vya siasa na wagombea huru wanne wanagombea viti, katika uchaguzi ambao chama cha Rais Paul Kagame - RPF, kinatarajiwa kunyakuwa idadi kubwa ya viti. Chama cha RPF kinashikilia asilimia 76 ya viti bungeni.

Jumapili, walemavu, na Wanyarwanda wanaoishi nchi za nje waliruhusiwa kupiga kura, leo wapiga kura wamewachagua wabunge 53, kesho itakuwa zamu ya kuwachagua wabunge wanawake 24, na wabunge vijana wawili.

Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa tarehe 16.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG