Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:26

Uchaguzi Misri kupima mafanikio, hasara zilizoletwa na mapinduzi


Wafuasi wa Rais Mohamed Morsi aliyeondoshwa madarakani nchini Misri.
Wafuasi wa Rais Mohamed Morsi aliyeondoshwa madarakani nchini Misri.

Miaka saba baada ya makundi ya watu wenye furaha kuandamana huko Cairo, Misri ikiwa ni harakati za kumwondosha madarakani mtawala wa muda mrefu Hosni Mubarak ambapo ilikuja kujulikana kama moja ya athari za mageuzi ya mapinduzi yaliyoletwa na vuguvugu la Arab Spring.

Misri hivi sasa inategemea kufanya uchaguzi wa urais Machi 2018 ambao utapima kile ambacho taifa hilo limefaidika kwalo na hasara zilizopatikana kutokana na siku kadhaa za misukosuko ya mapema mwaka 2011 baada ya kuondolewa madarakani Rais Mohamed Morsi.

Rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi alichaguliwa kuwa rais mwaka 2014, baada ya kumwondosha madarakani Rais Mohamed Morsi. Hivi sasa El Sissi anataka tena kuongoza kwa awamu nyingine. Baadhi ya wapiga hawakubaliani na hilo, wengine hawafurahi kabisa, lakini wako ambao wanataka aendelee kutawala.

Watu wa Misri walikuwa wanataka mageuzi hapo Januari 2011, na walifanikiwa kuyapata. Lakini miaka saba baadae, ukweli unaonyesha matumaini hayo kutoweka. Lakini baadhi ya wachambuzi wanasema mambo mengi yamebadilika kuwa bora zaidi.

Said Sadek wa Chuo Kikuu cha American University Cairo: “Kuna ukosoaji mkubwa juu ya rais, maafisa wa serikali, hivi leo ambao ilikuwa haiwezekani kukosoa, kwa mfano miaka 50 au 60 iliopita chini ya (utawala wa Rais wa zamani Gamal Abdel Nasser. Kwa hivyo Misri inapiga hatua, lakini usiilinganishe na kile kilichotokea katika nchi ambazo zilipitia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na karne kadhaa kujenga demokrasia zao.”

Kinyume na ilivyokuwa Syria na Libya, Misri ili jaribu kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo jeshi la nchi hiyo likizuia vurugu lakini wakati huo huo kukadamiza aina mbali mbali za uhuru mpya.

Said Sadek anasema: “ Sissi anajenga jeshi la Misri. Anafufua uchumi wa Misri, na miundo mbinu. Pia anajaribu kutatua matatizo sugu mbalimbali, kama vile kuongezeka kwa idadi ya watu.”

Lakini Misri imegawanyika, ambapo kikundi cha Waislam ambao wamekasirishwa na El Sissi kwa kupindua serikali ya chama cha Muslim Brotherhood. Wapiga kura wenye kupendelea mageuzi wanalalamika kupotea kwa baadhi ya uhuru wao. Wengi wanaamini kuwa Misri bado inalazimika kujiimarisha kutokana na mageuzi yaliyoletwa na vuguvugu la Arab Spring.

XS
SM
MD
LG