Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 17:54

Maswala ya Uhamiaji na Biashara yatawala kampeni za urais Marekani


Wagombea urais wa Marekani, Mrepublican Donald Trump na Mdemocract Hillary Clinton muda mfupi kabla ya mdahalo wa kwanza.

Hapo Novemba 8, wananchi wa Marekani watapiga kura kuchagua rais mpya atakayechukua nafasi ya rais Barack Obama ambaye anamaliza mihula yake miwili madarakani. Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa mkali katika nyanja mbali mbali ukiwapambanisha mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuwania urais – Hillary Clinton – kupitia chama cha Democratic na bilionea Donald Trump.

Katika swala la uhamiaji kama inavyofahamika Marekani ni taifa la wahamiaji – watu kutoka maeneo mbali mbali duniani – wapya na wa zamani - ambao wana mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na pia mchanganyiko wa utamaduni wa taifa hili. Lakini wagombea urais mwaka huu Donald Trump na Hillary Clinton w ana sera za uhamiaji zinazotofautiana kabisa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Lakini maendeleo kama vile mzozo wa wakimbizi huko Ulaya, tishio la ugaidi na kuwepo kwa takriban watu milioni 11 wanaoishi hapa Marekani kinyume cha sheria yamekuwa ni masuala makuu katika kampeni.

Na suala jingine kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu ni biashara, kuacha kufanya biashara na mataifa mengine. Hili ni moja ya masuala machache ya uchumi yanayowakabili wagombea wote wawili na Democratic na Republican.

Njia ya kuelekea White House inahitaji ridhaa ya wapiga kura kwa masuala mbali mbali, na masuala ya uhamiaji na usalama ndiyo masuala makuu katika uchaguzi wa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG