Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 00:08

Trump kufanya hotuba kuu badala ya mdahalo Jumatatu


Mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump.
Mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump.

Trump anapanga kufanya kile alichokiita hotuba kuu Jumatatu badala ya kufanya mdahalo na wapinzani wake wawili waliobaki kwa uteuzi wa chama chao.

Mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump, anasema anapanga kufanya kile alichokiita hotuba kuu Jumatatu badala ya kufanya mdahalo na wapinzani wake wawili waliobaki kwa uteuzi wa chama chao.

Trump alikuwa akitarajiwa kushiriki kwenye mdahalo wa shirika la habari la Fox huko Salt Lake City Utah, na Seneta wa Texas Ted Cruz na Gavana wa Ohio John Kasich, lakini alisema jana jumatano kwamba warepublikan wamepata midahalo ya kutosha na hatahudhuria.

Kasich naye alitangaza kwamba bila ya Trump kuwepo naye hatashiriki kutokana na kukosa washiriki, shirika la habari la Fox liliamua kufuta mdahalo huo.

Cruz yuko nyuma ya Trump kwa wajumbe 673 dhidi ya 410 alimshambulia mfanyabiashara huyo na kumwita Ducking Donald akimaanisha “anakwepa na kukimbia” na kuwaambia waunga mkono wake waende kwenye mtandao uitwao "duckingdonald.com."

XS
SM
MD
LG