Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:12

Upinzani Kenya wakubaliana kuwa na mgombea mmoja wa rais


Viongozi wa upinzani wa Kenya wakutana kupanga mkakati wa uchaguzi mkuu
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:16 0:00

Vyama vya upinzani nchini Kenya Jumatano vimeamua kumuunga mkono kiongozi mmoja kupeperusha bendera ya muungano na mageuzi ya kidemokrasia (CORD).

Katika juhudi za kumtafuta na kumtangaza mgombea urais pekee katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa Agosti 8, vyama vya upinzani vimekutana katika ukumbi wa kihistoria wa Bomas Kenya na kuamua kumuunga mkono kiongozi mmoja.

Vile vile viongozi hao wakiongozwa na kinara wa Orange Democratic Movement Raila Odinga, wameamwua kuwarai wafuasi wao kujisajili kupiga kura kwa wingi ili kumtoa rais Kenyatta madarakani.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA Kennedy Wandera amesema miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa, siasa zimeanza kunoga huku viongozi mbalimbali wa kisiasa wakianza kutafuta kuungwa mkono katika kura hizo lakini hivi sasa ni katika kambi za upinzani.

Wajumbe wa CORD wahudhuria mkutano wa Nairobi kupanga mkakati wa uchaguzi wa 2017
Wajumbe wa CORD wahudhuria mkutano wa Nairobi kupanga mkakati wa uchaguzi wa 2017

Ameelezea kuwa katika ukumbi wa Bomas hapa jijini Nairobi, wadau mbalimbali katika uchaguzi mkuu katika vyama tanzu vya CORD walikutana kufanya makubaliano muhimu kuhusu uchaguzi mkuu.

Ameongeza kuwa vyama hivi vya upinzani vikitarajiwa kuchukua msimamo mkali wa kisiasa kuhusu kupitishwa kwa marekebisho ya sheria za uchaguzi, wakenya wengi walitarajia kuwa upinzani ungerejea barabarani kuishinikiza serikali kuandaa mazungumzo nao.

Sheria hii inaruhusu mfumo wa kuhesabu kura kupitia mkono wakati wa uchaguziiwapo mitambo ya kielektroniki itafeli.

Akasema lakini badala yake, upinzani unaeleza kuelekeza juhudi hizo katika usajili wa wapiga kura kuwarai wakenya kujitokeza kwa wingi kushiriki mchakato huo kumuondoa kenyatta madarakani.

Upinzani ambao unajumuisha amani National Congress cha Musalia Mudavadi, Wiper Democratic Movement cha Kalonzo Musyoka, Orange Democratic Movement cha Raila Odinga, Ford Kenya kinara wake akiwa Moses Masika Wetangula pamoja na katibu mkuu wa Kanu Nick Salat unashikilia kuwa palikuwapo na hila katika kupitisha mswaada wa marekebisho ya sheria za uchaguzi katika mabunge yote.

Wajumbe wa upinzani kwenye mkutano wa CORD Nairobi, Kenya
Wajumbe wa upinzani kwenye mkutano wa CORD Nairobi, Kenya

Moses Wetangula ambaye pia kiongozi wa walio wachache katika bunge la Seneti amesema kiongozi wa Amani National Congress ambaye amekuwa akipiga debe sana kuhusu muungano maalum, uanojulikana kama National Super Alliance amewarai viongozi wenzake katika upinzani kusimama pamoja kumng'oa Kenyatta madarakani.

Lakini kile kilicho leta msisimuko katika ukumbi huo ni kauli ya kiongozi wa Wiper Democratic Movement Kalonzo Musyoka kuwa yuko tayari kumuachia kiongozi mwingine madaraka.

Kadhalika Odinga amewarai wa Kenya kujitokeza kwa wingi kujisajili ilikupiga kura kuiodosha serikali ya Jubilee madarakani.

XS
SM
MD
LG