Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:13

Polisi wakabiliana na waandamanaji Kisumu, Kibera


Polisi watupa bomu la machozi kwa waandamanaji
Polisi watupa bomu la machozi kwa waandamanaji

Marudio ya uchaguzi wa urais Kenya Alhamisi yameshuhudia vurugu kati ya polisi na waandamanaji, na pia kuwepo vituo vya kupiga ambavyo havikufunguliwa katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani.

Polisi walitupa bomu la machozi kwa waandamanaji huko eneo la Kibera, ambalo ni kitongoji cha Nairobi chenye vibanda vingi, wakati wapinzani wakijaribu kuweka vizuizi mbele ya kituo cha kupiga kura.

Vurugu pia zimetokea upande wa magharibi wa jiji la Kisumu, ambapo dazeni ya vituo vya kupiga kura vilikuwa vimefungwa na maafisa wa kusimamia kupiga kura hawajajitokeza.

Mtu mmoja Kisumu alipigwa risasi na kuuwawa wakati wa vurugu hizo kati ya polisi na waandamanaji, taarifa za polisi zimeeleza.

Marudio ya uchaguzi unafanyika baada ya zaidi ya miezi miwili baada ya Rais Uhuru Kenyatta kushinda uchaguzi ambao ulibatilishwa na Mahakama ya Juu kutokana na dosari na uvunjifu wa sheria katika kupeperusha matokeo uliofanywa na tume ya uchaguzi ya taifa inayojulikana kwa kifupi kama IEBC.

Lakini uchaguzi huo tayari umeingiliwa na utata. Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alijiotoa katika kinyang’anyiro hicho wiki mbili zilizopita, akidai kuwa IEBC ilikuwa haijafanya maboresho yoyote katika mchakato mpya wa uchaguzi, na amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi.

XS
SM
MD
LG