Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:24

Ubelgiji yaomba raia wake kuondoka Iran kwa ajili ya usalama wao


Maduka yaliofungwa Tehran kutokana na mgomo wa kitaifa
Maduka yaliofungwa Tehran kutokana na mgomo wa kitaifa

Serikali ya Ubelgiji Jumapili imewaomba raia wake waliopo Iran kuondoka nchini humo, ambako msako mkali unaendelea kutokana na maandamano ya kitaifa, kwasababu ya hofu kwamba huenda wakatiwa ndani kiholela.

Katika taarifa, serikali ya Ubelgiji imesema kwamba kuna hatari kubwa ya kukamatwa kwa wageni pamoja na wabelgiji wenye uraia pacha, kukiwa na hofu kwamba huenda wasipate haki baada ya kukamatwa.

Maafisa wa Ubelgiji wiki iliyopita walisema kwamba Iran ilitoa kifungo cha miaka 28 jela kwa mfanyakazi wa misaada, na kuzua mjadala mkali juu ya mpango wa kubadilishana wafungwa uliokwama kati ya mataifa hayo.

Ubelgiji imedai kuwa mfanyakazi aliyekamatwa nchini Iran hana hatia na kwamba ni mbinu ya taifa hilo ya kuishinikiza Ubelgiji kumuachilia mshukiwa wa ugaidi aliyefungwa Ubelgiji.

XS
SM
MD
LG