Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 17, 2025 Local time: 17:29

Ubelgiji inaiomba Afrika Kusini kutumia uhusiano wake na Russia kumaliza vita vya Ukraine


Mfalme wa Ubelgiji Philippe
Mfalme wa Ubelgiji Philippe

Ubelgiji Alhamisi imetoa wito kwa Afrika Kusini kutumia uhusiano wake na Russia ili kusaidia kumaliza vita nchini Ukraine, wito huo umetolewa katika ziara ya mfalme Philippe nchini humo.

“Kutokana na uhusiano wenu wa kihistoria ulio imara na Russia, tutafurahi ikiwa mtazingatia kutumia njia zenu za mawasiliano ili kusonga mbele kuelekea kupatikana kwa amani,” waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Hadja Lahbib amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria.

Lahbib ameambatana na mfalme Philippe na Malkia Matilde katika ziara yao ya kwanza ya kikazi ya siku tano nchini Afrika Kusini.

“Siku zote tumeiona Afrika Kusini kama mshirika mkuu kwa ajili ya amani na utetezi wa haki za binadamu,” Lahbib amesema.

Rais Cyril Ramaphosa amejibu kwa kusema kuwa Pretoria itaendelea kutumia “njia tuliyo nayo na Russia kuzungumzia jinsi mzozo huo unavyoweza kukomeshwa.”

Afrika Kusini ilikataa kulaani uvamizi wa Ukraine ambao ulipelekea Moscow kutengwa kwenye jukwaa la kimataifa, ikisema haitaki kuegemea upande wowote na inapendelea mazungumzo kumaliza vita hivyo.

XS
SM
MD
LG