Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 10:21

Ubalozi wa Uturuki wafunguliwa Somalia


Marais wa Somalia na Uturuki katika picha
Marais wa Somalia na Uturuki katika picha

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki na mwenzake wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, leo wamefungua rasmi ubalozi wa Uturuki nchini Somalia.

Msemaji wa Ikulu ya Somalia amedhibitishia shirika la habari la Somalia National News Agency kwamba marais hao wawili wamehudhuria hafa ya ufunguzi huo rasmi.

Mapema leo, Rais Erdogan aliwasili nchini Somalia, katika mkondo wake wa tatu na wa mwisho wa ziara yake ya Afrika Mashariki, kufungua miradi ambayo imedhaminiwa na serikali yake, ikiwa ni pamoja na taasisi za afya pamoja na ubalozi huo wake nchini Somalia, ambao ndio ubalozi wa Uturuki ulio mkubwa zaidi duniani.

Umuhimu wa Uturuki umeendelea kuonekana nchini Somalia, tangu ziara ya Erdogan ya mwaka wa 2011, wakati huo akiwa Waziri Mkuu, na ambayo ilikuwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa serikali ya Uturuki kuitembelea Somalia.

Ushirikiano kati ya Uturuki na Somalia umechangia mabadiliko mengi na kuimarisha hali ya afya na miundo msingi. Aidha makubaliano kadhaa kati ya nchi hizo mbili yametiwa saini, ikiwa ni pamoja na mkataba wa kuwapa mafunzo wanajeshi wa Somalia na kuanza kwa safari za ndege kati ya Ankara na Mogadishu.

XS
SM
MD
LG