Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:32

Aliyepigia kampeni kura ya Brexit hatawania uwaziri mkuu Uingereza


Boris Johnson
Boris Johnson

Mkonsavative mashuhuri aliechangia pakubwa kwenye kampeni ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Boris Johnson, amesema hatawania wadhifa wa Waziri Mkuu nchini humo.

Tangazo kwamba hatakuwa mgombea kwenye tiketi ya chama cha konsavative linaacha Waziri wa Sheria, Michael Gove, na mwenzake wa maswala ya nyumbani, Theresa May, waliounga mkono kura ya kubaki kwenye muungano, kama wagombea watakowania uongozi wa taifa hilo.

Johnson, ambae alikuwa Meya wa mji wa London, aliongoza kampeni ya kujiondoa kwenye muungano na wengi walitarajia kuwa angewania uongozi wa Uingereza wakati mpito wa kuondoka kwenye muungano huo wenye wanachama 28.

Waziri Mkuu atakaechaguliwa atakuwa na jukumu la kufanya mashauriano na Umoja wa Ulaya pamoja na jamii ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG