Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 15, 2025 Local time: 07:36

Twitter lazima iheshimu sheria za EU baada ya kunuliwa na Musk


Makao makuu ya Twitter mjini San Francisco. Oktoba 26, 2022
Makao makuu ya Twitter mjini San Francisco. Oktoba 26, 2022

Umoja wa Ulaya umesema kwamba Kampuni ya kimitandao ya Twiter itahitaji kufuata sheria za umoja huo, baada ya kununuliwa na tajiri Elon Musk, anayedai kuwa mwanaharakati wa uhuru wa kujieleza.

Musk ameanidka ujumbe wa Titwer kwamba ‘ndege yupo huyo’, akiwa na maana ya kwamba Twiter, ambayo alama yake ya biashara ni picha ya ndege, ipo huru kufanya kazi zake bila kudhibitiwa.

Musk amenunua kampuni ya twiter kwa gharama ya dola bilioni 44 za kimarekani. Mkuu wa biashara wa umoja wa Ulaya Theirry Breton, amejibu ujumbe wa Musk akisema kwamba kampuni yeyote inayofaanya kazi ulaya lazima iheshimu sheria za umoja huo.

Mojawapo ya hatua ambazo Musk amechukua ni kufuta kazi wafanyakazi wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo. Miongoni mwa wale ambao wamefutwa kazi ni mkurugenzi mkuu Parag Agrawal, Afisa mkuu wa fedha Ned Segal na mshauri wa sheria na sera Vijaya Gadde.

Musk amekuwa akishutumu maafisa hao kwa kile amedai kwamba kukosa kumpa taarifa za uhakikika kuhusu idadi ya akaunti feki kwenye mtandao wa Twiter. Kampuni ya twiter ina karibu wafanyakazi 7,500 ambao sasa hawana uhakika iwapo watendelea kufanya kazi kwenye kampuni hiyo.

Musk amesema kwamba anatapanga kupunguza idadi ya wafanyakazi katika juhudi za kujenga mtandao mzuri zaidi. Kampuni ya twiter inapanga kupanua huduma zake na kuhusisha biashara kwenye mtandao kama kununua bidhaa na hata kulipia nauli ya magari ya kukodisha.

XS
SM
MD
LG