Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:16

Twitter yatimiza miaka kumi


Mtandao huo ambao una mamilioni ya watu ambao wametokea kuupenda na kuujua hauna mpango wa kuongeza tarakimu za uandishi wake kuzidi 140.

Mtandao wa Twitter leo umefikisha miaka 10. Mtandao huo ambao una mamilioni ya watu ambao wametokea kuupenda na kuujua hauna mpango wa kuongeza tarakimu za uandishi wake kuzidi 140.

Kila siku watumiaji wa Twitter wanaiambia dunia mambo makubwa katika maisha yao.

Biashara kubwa kubwa na ndogo ndogo zimejiunga na mtandao huo na kutoa maelezo mbali mbali kuhusu biashara zao.

Twitter pia umekuwa mtandao wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii, vugu vugu la nchi za kiarabu la mwaka 2011 liliutumia sana mtandao huu kupeana taarifa juu ya yale yaliokuwa yakiendelea.

XS
SM
MD
LG