Ma-super star wa Hollywood wanakusanyika leo Jumapili kusherehekea maonyesho bora ya filamu katika tuzo za kila mwaka za Academy, sherehe inayotarajiwa kugeuka kuwa sherehe ya kuwanadi waigizaji wa filamu kabambe ya “Oppenheimer”.
Mtangazaji katika kipindi cha Talk Show, Jimmy Kimmel anarudi kwa mara ya nne katika kusheherehesha tuzo za heshima kubwa katika tasnia ya filamu zinazofanyika kutoka ukumbi wa Dolby huko Los Angeles nchini Marekani.
“Oppenheimer,” filamu ya saa tatu iliyoongozwa na Christopher Nolan inaongoza kwenye jukwaa kwa kuteuliwa mara 13. Filamu hiyo inaongoza katika ushindi wa kipengele cha picha bora zaidi, ikishinda tuzo nyingine kubwa mwaka huu.
Forum