Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 13:11

HRW yaitisha uchunguzi dhidi ya mauwaji ya raia huko Cizre, Uturuki.


Wanajeshi wa Uturuki wakipiga doria mjini Cizre.
Wanajeshi wa Uturuki wakipiga doria mjini Cizre.

Shirika la kutetea haki za binadam lenye makao yake Marekani, limeishutumu Ankara kwa kuzuia uchunguzi wa kimataifa dhidi ya kile walichokiita ukiukaji mkubwa wa haki za binadam unaofanywa na vikosi vya usalama katika ukandamizaji wao wa waasi wa Kikurdi.

Ripoti hiyo ya shirika la human rights watch ililenga mapigano baina ya wanajeshi wa usalama wa Uturuki na waasi wa Kikurdi huko Cizre. Mji huo ni kitovu cha uzalendo wa Kikurdi ambao umeshuhudia baadhi ya mapigano makali tangu kuvunjika mwaka jana kwa utaratibu wa Amani na kundi la waasi wa Kikurdi la PKK.

Mwandishi wa ripoti hiyo ya Human Rights Watch, Emma Sinclair Webb, anatuhumu wanajeshi wa usalama wanafunika ukiukaji wa haki unaofanyika huko.

Bi Sinclair anasema, kuna idadi kubwa za raia ambao wameuwawa wakati wa operesheni za usalma. Na hakuna ishara ya kuchunguzwa kwa vifo hivyo, bali, kuna juhudi za kuficha. Tunazuiwa kutembelea familia ambazo zimepoteza jamaa zao wakati wa operesheni za usalama.

Wanajeshi wa usalama wa Uturuki wanasema, hamna raia walouwawa katika operesheni za takriban miezi 10 za kijeshi dhidi ya PKK, lakini Sinclair Webb anasema, wengi wa raia waloathiriwa ni miongoni mwa raia walokudhaifu Zaidi.

Bi Sinclair anasema, Ince alikuwa mtoto wa umri wa miezi 3, ambaye shangazi yake alikuwa akimbeba kumpeleka chini nyumbani mwao, pale alipopigwa risasi na wanajeshi walokuwa wamejitweka mlimani, na kwenye magari ya kijeshi, kulingana na familia. Na katika juhudi za kumpeleka mtoto hospitali, familia hiyo iliendesha gari wakiwa huku wamepeperusha bendera nyeupe, na kwa mara nyengine tena, walishambuliwa kutoka eneo la mlimani, na wote mtoto na babu yake waliuwawa.

Serikali imesema kuwa madai ya ukiukaji utachunguzwa. Ripoti ya human Rights watch pia ilimulika sehemu kubwa za mji wa Cizre ulowashwa moto. Serikali inasema nyumba zote ziliharibiwa zitajengwa tena.

Sinclair Webb pia anasema kuna ushahidi wa mauwaji ya watu takriban 130 wanaotafuta hifadhi kutokana na mapigano hayo.

Hapo Mwezi Mei, kamishna wa umoja mataifa wa haki za binadam Zeid Ra’ad al Hussein aliitisha Ankara kuruhusu uchunguzi wa mauwaji katika nyumba , wito ambao umekataliwa. Serikali inakana mashtaka ya mauwaji, ikisema matukio yalopelekea mauwaji hayo hayako bayana.

Human Rights Watch imeunga mkono wito wa umoja mataifa wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa.

​
XS
SM
MD
LG