Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 23:07

Uturuki yarejea katika hali ya kawaida


Bendera zapepea nusu mlingoti nchini Uturuki
Bendera zapepea nusu mlingoti nchini Uturuki

Uturuki inarejea katika hali ya kawaida baada ya wajitoa muhanga kushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk mjini Istanbul katika shambulizi ambalo waziri mkuu wa Uturuki anasema limeuwa takriban watu 41 ikiwa ni pamoja na watu 13 ambao ni raia wa nchi za nje na takriban wengine 250 kujeruhiwa.

Bendera kote nchini Uturuki zilipeperuka nusu mlingoti Jumatano pale taifa hilo lilipoadhimisha siku ya maombolezi kufwatia shambulizi la wajitoa mhanga 3 Jumanne katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk mjini Istanbul. Wanusura wamekuwa wakieleza yale waloshuhudia na kutuma ujumbe wa ujasiri, Kama msafiri kutoka Hungary, Dorka Kardosh.

Kardosh alisema, anadhani hatupaswi kuwa waoga kwa sababu hilo ndilo lengo lao, lakini hatuwezi kuishi maisha yetu tukiogopa kwenda nje.

Wafatiliaji wanasema mamlaka za Uturuki zimehakikisha kutuma ujumbe kuwa Istanbul bado ni jasiri. Masaa tu baada ya mashambulizi, uwanja wa ndege wa Ataturk ulifunguliwa tena. Vikosi vya usalama vya Uturuki viko katika harakati za kuwatambulisha wajitowa mhanga hao. Washambuliaji wanaonekana kuwa walijiandaa na kujiratibu vyema. Kabla ya kujiripua, washambuliaji walokuwa wamejihami vyema, walishambulia watu kwa bunduki na bastola katika eneo la kuwasili abiria wakimataifa, ambalo lilikuwa limejaa watu.

Uwanja wa ndege wa Ataturk ni mojawapo ya viwanja vya ndege vilivyo na shughuli nyingi duniani. Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yidirim, akizungumza baada ya shambulizi, alililaumu kundi la Islamic state.

Kwa mujib wa taarifa za awali kutoka kwa maafisa wa uslama wa Uturuki, shambulizi linaonekana kuwa limefanywa na kundi la Daesh, ambalo ni jina jengine la kundi la Islamic State. Mkuu wa shirika la kijasusi la Marekani John Brennan alisema Jumatano kuwa shambulizi hilo linaonyesha ishara za kile alichokiita uasi wa Islamic State.

Bw Yildirim alitowa wito wa umoja wa kitaifa, lakini wafatiliaji wanaonya kuwa shambulizi huwenda likazidisha migawano ya kisiasa. Vyama vya upinzani vinaishutumu serikali kwa kushindwa kupambana zaidi na kundi la Islamic state ambalo linaaminiwa kuwa na mtandao mkubwa nchini humo.

Vituo vya habari vinaripoti kuwa idara ya kijasusi ya Uturuki ilitowa onyo wiki kadhaa zilizopita kuwa Istanbul inakabiliwa na kitisho cha shambulzi kutoka kwa Islamic State. Wachambuzi wanasema kundi hilo la wanajihadi ambalo limekosa ushindi wa kijeshi huko Iraq na Syria ,litakuwa na ari ya kufanya shambulizi la kulipiza kisasi. .

XS
SM
MD
LG