Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 04:11

Chama tawala cha Uturuki, AKP chapata mkuu mpya


Binali Yildirim
Binali Yildirim

Erdogan ametangaza azma yake ya kusukuma mageuzi ya katiba kuubadili mfumo wa nchi kutoka demokrasia ya bunge na kuwa na utendaji wa urais huku kukiwa na kanuni chache za ufuatiliaji.

Mshirika wa karibu wa rais wa uturuki, Recep Tayyip Erdogan amechaguliwa kiongozi wa chama tawala nchini humo, na hivyo kuwa waziri mkuu mtarajiwa. Hatua hiyo inaonekana kama hatua ya karibuni ya rais kuimarisha zaidi madaraka yake na kuifanya Uturuki kuwa serikali yenye rais mtendaji.

Maelfu ya wanachama wa chama tawala cha Uturuki AKP walijazana katika ukumbi wa mkutano mjini Ankara kumchagua bila ya kupingwa Binali Yildirim kama kiongozi wake mpya na waziri mkuu mtarajiwa. Bw Yildrim ambaye ni waziri wa usafiri ni mmoja wa washirika wa karibu na wa mda mrefu rais Erdogan.

Yildirim aliahidi kutekeleza matarajio ya rais wake.

Bw Yildirim anasema kazi muhimu kwa serikali inayotakiwa kufanya ni kupitisha katiba mpya na kubadili katiba kwa mfumo wa urais

Erdogan ametangaza azma yake ya kusukuma mageuzi ya katiba kuubadili mfumo wa nchi kutoka demokrasia ya bunge na kuwa na utendaji wa urais huku kukiwa na kanuni chache za ufuatiliaji.

Wakosoaji wanasema hilo litakuwa kama udikteta wa kuteuliwa.

Wafatiliaji wanasema waziri mkuu anayeondoka madarakani, Ahmed Davatoglu, ambaye alijiuzlu rasmi kutoka wadhifa wake Jumapili, anaaminika kuwa alipinga mabadiliko kama hayo na hivyo kupelekea kuondolewa na rais, ingawaje amewahi kuwa mshirika wake wa karibu.

Mkutano wa jana wa chama tawala ulikuwa na hamu kuwasilisha ujumbe muhimu wa umoja na kuwa hakuna dalili za wazi wazi za uasi. Lakini pembeni, wafuasi wa waziri mkuu aliyeondolewa mamlakani wameripotiwa kuondolewa kwenye nafasi zao katika chama.

Washirika wa Nato wa Ankara ambao wanaiangalia Uturuki kama mshirika muhimu katika vita dhidi ya Islamic State wamezidisha kutoa sauti za wasi wasi kwamba Erdogan anajaribu kuwa mtawala wa kimabavu.

Wasiwasi huo huwenda ukaongezeka kufuatia kuondolewa kwa waziri mkuu aliyepita, Dovatoglu ambaye alionekana kuwa na athari ya wastani kwa rais.

XS
SM
MD
LG