Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:05

Waturuki wataka mshukiwa wa mapinduzi kuhamishwa Marekani


Fethulla Gulen
Fethulla Gulen

Kundi la wabunge kutoka Uturuki liko hapa Wahington kushinikiza maafisa wa serikali ya Marekani kukubali ombi la serikali ya Ankara kutaka imamu wa zamani ambaye anatuhumiwa kupanga jaribio la kuipidua serikali ya Uturuki arudishwe nyumbani.

Kamil Aydin, mbunge kutoka chama cha kizalendo cha mrengo wa Kulia cha National Movement Party, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba wangetaka kuona Marekani ikichukua hatua za dhati dhidi ya Fethullah Gulen na inaponyamaza kuhusiana na ombi la itamhamisha. Alisema Uturuki ingetaka awekwe kizuizini au shughuli zake za kila siku kudhibitiwa.

Aydin na wabunge wengine watatu kutoka Uturuki walikutana na maafisa wa serikali ya Marekani katika waizara ya Sheria jana Jumatatu, kabla ya kuondoka na kwenda kufanya mazungumzo katika wizara ya usalama wa ndani na baadaye, wizara ya mambo ya nje.

XS
SM
MD
LG