Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 19, 2025 Local time: 21:08

Mashambulizi ya anga yaanza tena dhidi ya ISIS kutoka Uturuki

Kituo cha kijeshi cha Incirlik Uturuki.
Kituo cha kijeshi cha Incirlik Uturuki.

Mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani kutoka Uturuki yameanza tena dhidi ya kundi ya Islamic State hata baada ya anga ya chi hiyo kufungwa kufuatia jaribio la mapinduzi la Ijumaa.

Mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani kutoka Uturuki yameanza tena dhidi ya kundi ya Islamic State hata baada ya anga ya chi hiyo kufungwa kufuatia jaribio la mapinduzi la Ijumaa.

Mashambilizi hayo yalikuwa yamepigwa marufuku kwa muda na serikali ya Uturuki. Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesesema kuwa mamlaka ya Uturuki imefungua anga yake tena kwa ndege za kijeshi Jumapili. Uturuki ambayo ni rafiki wa muda murefu wa Marekani imeruhusu Marekani kutumia kituo cha kijeshi cha Incirlik kilichoko kwenye mji wa Adana kurushia silaha dhidi ya Islamic State.

Wakati huo huo,serikali ya Uturuki imemzuilia kamanda wa kituo hicho cha Incirlik generali Bekir Ercan Van pamoja na wanajeshi wengine 10 na polisi mmoja kwa kushukiwa kuhusika kwenye jaribio la mapinduzi lililotibuka.

XS
SM
MD
LG