Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 16:59

Uturuki yaionya Syria kuacha mashambulizi kwa raia wake


Moja ya vifaru vya jeshi la Syria katika mitaa ya mji wa Hama ambapo jeshi linawadhibiti waandamanaji wanaoipinga serikali ya Rais Bashar al-Assad
Moja ya vifaru vya jeshi la Syria katika mitaa ya mji wa Hama ambapo jeshi linawadhibiti waandamanaji wanaoipinga serikali ya Rais Bashar al-Assad

Uturuki imeionya Syria kuacha oparesheni zake za kijeshi dhidi ya raia wake mara moja na bila masharti.

Uturuki imewaonya jirani zake nchi ya Syria kwamba oparesheni zake za kijeshi dhidi ya raia lazima zisitishwe mara moja na bila masharti.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Ahmed Davutoglu alisema kwa maneno yake, haya ni maneno yetu ya mwisho kwa maafisa wa Syria. Alizungumza na waandishi wa habari huko Ankara wakati jeshi la Syria liliporipotiwa kufanya mashambulizi katika maeneo ya makazi katika mji wa bandari wa Latakia.Ilikuwa siku ya tatu ya shambulizi dhidi ya upinzani unaoipinga serikali huko.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Syria wanasema majeshi ya usalama yamewauwa watu wasiopungua 30 katika mji wa pwani tangu Jumamosi ikiwemo miji miwili siku ya Jumatatu. Mashahidi huko Latakia wanasema watu wanajaribu kukimbia, lakini kwamba watu kadhaa wamepigwa risasi katika vituo vya ukaguzi.

Huko Houla mji mmoja karibu na mji wa Homs, wanaharakati wanasema majeshi ya Syria yaliyokuwa kwenye vifaru yamefanya mashambulizi na ukamataji. Latakia na Homs ni miongoni mwa miji ya Syria ambayo imekuwa na waandamanaji wengi wanaodai kujiuzulu kwa Rais Bashar al-Assad.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alimtembelea Rais Assad huko Damascus wiki iliyopita kumsihi kumaliza ukamataji wake dhidi ya ghasia za waandamanaji wanaoipinga serikali. Bwana Davutoglu alisema Jumatatu kwamba inabidi umwagaji damu usitishwe mara moja, hakutakuwa na kitu chochote cha kuzungumza na utawala wa Syria.

Shirika moja la Umoja wa Mataifa linasema ghasia huko Latakia zimewalazimisha kiasi cha wa-Palestina 5,000 kukimbilia kwenye kambi moja ya wakimbizi katika eneo la kusini ya mji. Umoja wa Mataifa unaelezea wasi wasi kuhusu hali hiyo.

XS
SM
MD
LG