Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:01

Tunisia yaunda serikali ya mseto


Hammadi Jebali, katibu mkuu wa chama cha Ennahda, atachukua nafasi ya uwaziri mkuu.
Hammadi Jebali, katibu mkuu wa chama cha Ennahda, atachukua nafasi ya uwaziri mkuu.

Hamadi Jebali kutoka chama cha kiislam cha Ennahda atachukua nafasi ya waziri mkuu katika serikali ya ushirikiano wa madaraka.

Vyama vikuu vitatu vya kisiasa nchini Tunisia ambavyo viliunda serikali ya mseto Jumatatu vilitangaza makubaliano ya kushirikiana madaraka katika ngazi tatu za juu serikalini. Katika makubaliano hayo Hamadi Jebali kutoka chama cha kiislam cha Ennahda ambacho kilipata kura nyingi katika uchaguzi uliopita wa bunge atachukua nafasi ya waziri mkuu. Mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto wa chama cha Republikan , Moncef Marzouki atakuwa rais mpya na Mustafa Ben Jafaar wa Ettakatol atakuwa spika mpya wa bunge ambalo linajukumu la kuandika katiba mpya.

XS
SM
MD
LG