Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:49

Tunisia yakaribia kupata mkopo wa IMF


Maandishi ya IMF kwenye ofisi za makao makuu, Washington DC
Maandishi ya IMF kwenye ofisi za makao makuu, Washington DC

Gavana wa benki kuu ya Tunisia Marouan Abassi amesema Jumapili kwamba taifa lake linatarajia kufikia makubaliano na IMF ndani ya wiki kadhaa zijazo kuhusu mkopo wa kati ya dola bilioni 2 na 4 za kimarekani utakaotolewa ndani ya miaka mitatu.

Tunisia ambayo inapitia hali ngumu kiuchumi inahitaji mkopo wa IMF, ili kuzuia kuporomoka kwa uchumi wake. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Abassi amesema kwamba kiwango cha mkopo kinaendelea kujadiliwa lakini huenda kikawa kati ya dola bilioni 2 na 4 za kimarekani.

Serikali na muungano wa kitaifa wa wafanyakazi wenye nguvu wa UDTT wiki iliyopita walisaini mkataba wa nyongeza ya asilimia 5 kwenye mishahara, ikiwa kama hatua ya kupunguza taharuki ya kiuchumi nchini. Hata hivyo serikali haikutangaza hatua zaidi za marekebisho ambazo zinahitajika na IMF kabla ya mkopo kutolewa.

IMF hapo awali ilisema kwamba haingetoa mkopo kwa Tunisia hadi serikali ifanye makubaliano na muungano wa UGTT wenye zaidi ya wafanyakazi milioni moja kote nchini. UGTT mara kadhaa umesimamisha uchumi wa taifa hilo mara kadhaa kupitia migomo ya kitaifa.

XS
SM
MD
LG