Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:20

Tunisia yagubikwa na maandamano ya kumpinga Rais


Polisi wa kutuliza ghasia akikutana uso kwa uso na waandamanaji katika mji mkuu Tunis, Tunisia, 18 Jan 2011
Polisi wa kutuliza ghasia akikutana uso kwa uso na waandamanaji katika mji mkuu Tunis, Tunisia, 18 Jan 2011

Januari 14 ni kumbukumbu ya mapinduzi ya kidemokrasia ya Tunisia mwaka 2011 wakati maandamano yalipolazimisha rais wa zamani wa kiimla Zine al- Abidine Ben Ali kuondoka madarakani. Upinzani bado umegawanyika Jumamosi, kama Saied aondolewe madarakani .

Makundi kadhaa yaliandamana Jumamosi ingawa polisi ilisema wanapaswa kuandamana katika maeneo tofauti na Tunis. Hata hivyo walikaidi maagizo ya polisi na kuandamana hadi barabara ya Habib Bourguiba katikati mwa mji eneo la kitamaduni la mikutano .

Waandamanaji walipita kwenye vizuizi vya polisi na kupuuza amri zao licha ya kwamba walikuwa na mipira ya maji iliyokuwa imewekwa mahali ambayo watu walikusanyika.

Saied alivunja bunge lililochaguliwa mwaka 2021 na kuanza kufanya mabadiliko ya kiholela kwa mfumo wa kisiasa lakini uchaguzi wa wabunge wa Desemba ulionyesha uungwaji mkono mdogo wa umma kwa mabadiliko yake.

Makundi makubwa ya kisiasa na jumuiya ya wafanyakazi wanapinga mabadiliko hayo ambayo Saeid ana mpango wa kuyatekeleza, huku wengi wanabashiri mapinduzi ya kidemokrasia.

Hata hivyo jumuiya bado zimegawanyika sana katika kufanya kazi pamoja zikimpinga rais.

XS
SM
MD
LG