Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:43

Raia wa Tunisia ahusishwa na shambulizi la Berlin


Sehemu ya soko linalouza bidhaa za krismas mjini Berlin ambalo lilivamiwa na lori na kusababisha vifo vya watu 12 kadhaa kujeruhiwa.
Sehemu ya soko linalouza bidhaa za krismas mjini Berlin ambalo lilivamiwa na lori na kusababisha vifo vya watu 12 kadhaa kujeruhiwa.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere amesema hakuna shaka shambulizi la lori la Jumatatu lilikuwa limepangwa.

Serikali ya Ujerumani imeendelea kumsaka dereva aliyeliendesha lori kwa spidi ya juu ndani ya Soko la bidhaa za krismas mjini Berlin lililokuwa limejaa watu, siku moja baada ya kumwachia huru mtu aliyekuwa amekamatwa muda mfupi baada ya shambulizi hilo lililo uwa watu 12.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimesema polisi bado wanaendelea na msako raia mmoja wa Tunisia ambaye nyaraka zake zilipatikana ndani ya lori.

Polisi mjini Berlin wanasema wamepata zaidi ya fununu 500 kwa njia ya simu tangu tukio hilo litokee Jumatatu.

Hata hivyo Islamic State imedai kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa kufuatia maagizo waliyotoa kwamba watu wawashambulie raia wa nchi zilizo katika ushirika unaoongozwa na Marekani unaotaka kuwaangamiza wapiganaji hao.

Ujerumani siyo katika nchi ambazo zinaendesha mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya Islamic State nchini Iraq na Syria, lakini imekuwa ikitoa msaada kwa ushirika wa Marekani ikiwemo kuwapa mafuta na taarifa za kijasusi.

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ambaye aliweka shada la maua meupe kwenye eneo la shambulizi hilo nje ya sehemu maarufu ya Kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial Jumanne, alisema ameshtushwa na kusikitishwa sana na tukio hili.

“Watu 12 ambao walikuwa na sisi mpaka hivi juzi, ambao walikuwa na shauku ya kusherehekea krismas, na walikuwa na mipango ya sikukuu, hawako nasi tena,” alisema katika taarifa aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa. “Kitendo cha kinyama na kisichokubalika kimenyang’anya maisha ya watu hawa.”

XS
SM
MD
LG