Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 23:40

Tunisia ilipata miili 901 ya wahamiaji waliokufa maji mwaka huu


Maiti za wahamiaji zilizofunikwa katika mji wa bandari wa Sfax, nchini Tunisia, Disemba 24, 2020.
Maiti za wahamiaji zilizofunikwa katika mji wa bandari wa Sfax, nchini Tunisia, Disemba 24, 2020.

Walinzi wa pwani ya Tunisia walipata miili 901 ya wahamiaji waliokufa maji katika pwani ya nchi hiyo kuanzia Januari 1 hadi Julai 20 mwaka huu, waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Kamel Feki alisema Jumatano.

Taifa hilo la Afrika Kaskazini linashuhudia wimbi kubwa la uhamiaji mwaka huu na majanga ya mara kwa mara ya kuzama kwa maboti ya wahamiaji kutoka nchi za Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wakielekea kwenye pwani za Italia.

Tunisia imechukua nafasi ya Libya kama kituo kikuu cha kuanzisha safari kwa watu wanaokimbia umaskini na mizozo barani Afrika na Mashariki ya Kati kwa matumaini ya kuwa na maisha bora barani Ulaya.

Feki aliliambia bunge kwamba miongoni mwa miili 901 iliyopatikana, 36 ilikuwa ya Watunisia na 267 ya wahamiaji wa kigeni, huku uraia wa waliobaki ukiwa haujulikani.

Boti nyingi zinazosafirisha wahamiaji huondoka kutoka pwani ya mji wa kusini mwa Tunisia wa S-Fax.

Maelfu ya wahamiaji wasio na vibali walifurika katika mji wa pwani wa Sfax katika miezi ya hivi karibuni kwa lengo la kuelekea Ulaya kwa kutumia boti zinazoendeshwa na wasafirishaji haramu wa binadamu, na kusababisha mzozo wa uhamiaji ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Tunisia.

Zaidi ya boti 75,000 za wahamiaji zilifika Italia tarehe 14 Julai, ikilinganishwa na zaidi ya boti 31,000 katika kipindi hicho hicho mwaka jana, takwimu rasmi zimeonyesha. Zaidi ya nusu ya boti hizo ziliondoka kutoka Tunisia.

Umoja wa Ulaya na Tunisia walisaini makubaliano ya kimkakati mwezi huu wa Julai ambayo yanajumuisha kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu na kuimarisha usalama kwenye mipaka ya bahari wakati kukiwa na ongezeko kubwa la boti zinazoondoka kutoka taifa hilo la Afrika Kaskazini, zikielekea Ulaya.

Forum

XS
SM
MD
LG