Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:33

Serikali ya Tunisia yawatia mbaroni washukiwa wa shambulizi la Berlin


Nour, mama yake mtuhumiwa wa shambulizi la bomu kwenye soko la krismas, Berlin, Ujerumani. Nour yuko Oueslatia, Tunisia.
Nour, mama yake mtuhumiwa wa shambulizi la bomu kwenye soko la krismas, Berlin, Ujerumani. Nour yuko Oueslatia, Tunisia.

Ujerumani inaendelea na zoezi la kuwasaka wote walioshirikiana na mshukiwa wa shambulizi la lori kwenye soko la bidhaa za krismas mjini Berlin.

Vyombo vya usalama nchini Tunisia vimemkamata mpwa wa mshukiwa wa shambulizi la soko la krismas la mjini Berlin, Anis Amri, pamoja na wanamgambo wa kiislamu wawili wanaoshukiwa pia “kuwa na mahusiano” na Amri, wizara ya mambo ya ndani imesema leo Jumamosi.

Washukiwa hawa watatu wanasadikiwa kuwa ni wanachama “wa kikundi cha kigaidi… chenye mahusiano na gaidi Anis Amri aliyefanya shambulio la kigaidi mjini Berlin,” ilisema taarifa hiyo. Wote wawili walitiwa nguvuni siku ya Ijumaa.

Wakati huo huo mamia ya watu mjini Tunis walijitokeza mitaani siku ya Jumamosi wakilaani vitendo vya kigaidi .

Takriban watu 200 walishiriki katika maadamano hayo na kuitaka serikali kuwarejesha raia wote wa Tunisia nchini ambao wana mahusiano na vikundi vya kigaidi, ili waweze kushtakiwa nchini humo.

Maandamano hayo yalikusanyika nje ya jengo la makumbusho la Bardo, mahali ambako shambulizi la kigaidi lilifanyika mwaka jana na kundi la Islamic State kudai limehusika.

Mtu mwenye silaha aliuwa watu 22 katika shambulizi la Mwezi Machi 2015 – wakiwemo watalii wa kigeni 21 na askari wa Tunisia.

XS
SM
MD
LG