Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 14:13

Amani na usalama vidumishwe Afrika - Macky Sall


Rais wa Senegal, Macky Sall akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York. .
Rais wa Senegal, Macky Sall akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa New York. .

Viongozi wengi wa bara la Afrika kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walitumia hotuba zao kwenye taasisi hiyo ya dunia kuelezea wasi wasi wao kuhusu kuongezeka kwa tishio la ghasia za wenye msimamo mkali huko Afrika.

Viongozi kadhaa kutoka bara hilo waliiomba jumuiya ya kimataifa kusaidia kuvipatia vifaa vikosi vya kieneo dhidi ya ugaidi ili kupambana na ugaidi hususan wakati wanajihadi waliposhindwa huko mashariki ya kati wakati kundi la Islamic State-IS linapoteza nguvu na mamlaka katika eneo watarudi kwenye makazi yao katika nchi za Afrika.

Rais wa Senegal, Macky Sall.
Rais wa Senegal, Macky Sall.

“Tunaitaka Afrika iwe katika amani na usalama, Afrika ambayo haitumiki kama hifadhi ya makundi ya ugaidi yaliyopambana na kushindwa kwingineko” Rais Macky Sall wa Senegal aliwaambia siku ya Jumatano viongozi wa dunia waliokusanyika kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika kila mwaka huko New York nchini Marekani.

Lakini utafiti mpya uliofanywa na program ya maendeleo katika Umoja wa Mataifa-UNDP mwezi huu umegundua kwamba hatua zilizochukuliwa na serikali za kiafrika kupambana na ugaidi zinawasukuma watu wengi zaidi kujiunga na makundi ya ghasia.

XS
SM
MD
LG