Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:50

Tunabusu mikono ya aliyepanga mashambulizi dhidi ya Israel - Kiongozi wa Iran, Ayatollah Khemenei


Mwanamme akiomboleza kwenye kaburi mjini Jerusalem Okt 9 2023
Mwanamme akiomboleza kwenye kaburi mjini Jerusalem Okt 9 2023

Iran, ambaye inaunga sana mkono kundi la Hamas, limefurahishwa na shambulizi la Jumamosi lakini imekanusha madai kwamba inahusika.

Kiongozi wa juu wa Iran Ali Khamenei alisema Jumanne kwamba Iran imebusu mikono ya waliopanga shambulizi hilo, na kwamba mtu yeyote aliyedhani kwamba Iran inahusika na shambulizi hilo, anakosea.

Shambulizi baya kwenye mpaka wa kaskazini na Israel mnamo Jumatatu limepelekea wasiwasi wa kutoka vita vibaya kati ya Israel na kundi lingine la Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran.

Hezbollah limesema kwamba halihusiki na shambulizi dhidi ya Israel.

Mkuu wa jeshi wa ngazi ya juu wa Marekani Generali Charles Q. Brown, ameonya Iran dhidi ya kujihusisha na vita vinavyoendelea.

Wanajeshi wa Israel wamezingira Gaza

Israel imesema leo Jumanne kwamba imedhibithi mpaka wa Gaza, na kushambulia kwa makombora kadhaa sehemu hiyo ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika muda wa miaka 75 ya vita vyake na Palestine, licha ya kundi la Hamas kutishia kuua watu ambao limewateka nyara.

Israel imeapa kulipiza kisasi tangu watu wenye bunduki walipovamia miji ya Israel na kusababisha vifo kadhaa katika shambulizi ambalo limetaja kuwa baya sana katika historia.

Jeshi la Israel limeagiza maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kushiriki katika oparesheni dhid ya Hamas, na kuweka ukanda wa Gaza chini ya udhibithi wake.

Sehemu hiyo ina watu milioni 2.3.

Vyombo vya habari vya Israel vimesema kwamba idai ya kifo kutokana na shambulizi la kundi la Hamas imefikia watu 900, wengi wao wakiwa raia waliopigwa risasi na kuuawa nyumbani kwao, barabarani na waliokuwa katika sherehe.

Idadi hiyo ya vifo ni kubwa Zaidi kuwahi kutokea kutokana na shambulizi la kigaidi, kando la shambulizi la 9/11.

Karibu watu 700 wameuawa katika ukingo wa Gaza kutokana na mashambulizi ya Israel. Idadi hiyo ya vifo imetolewa na maafisa wa Gaza. Karibu wilaya nzima ndani ya Gaza imeharibiwa vibaya.

Umoja wa mataifa umesema kwamba watu 180,000 katika Gaza hawana makao, wengi waoa wanakaa kando ya barabara au shuleni.

Juhudi za uokoaji zimeathiriwa na mashambulizi ya makombora yanayoendelea.

Hawana pa kujificha - Jeshi la Israel

Waandishi watatu katika ukingo wa Gaza wameuawa baada ya kombora la Israel kugonga jingo ambalo walikuwa wanafanyia kazi.

Kufikia sasa, waandishi sita wa habari wameuawa tangu Jumamosi.

Wakati mmoja, jeshi la Israel lilishauri raia kukimbilia Misri, lakini baadaye likafafanua kwamba mpaka ulikuwa umefungwa na hakuna mtu angetoka Gaza.

Msemaji wa jeshi Admiral Daniel Hagari, amesema kwamba wapiganaji wa Hamas “hawana pa kujificha”, akiongezea kwamba “tutawafikia popote walipo.”

Nchini Israel, hakuna idadi rasmi ya vifo kutokana na shambulizi la Hamas.

Katika mji wa kusini wa Be’eri ambapo Zaidi ya miili 100 imepatikana, wafanyakazi wa kujitolea wamebeba miili hiyo na kupeleka katika vyumba vya kuhifadhi maiti.

Jeshi la Israel limezunguka Gaza, Hamas limetishia kuua mateka

Msako wa kijeshi katika Gaza

Jeshi la Israel linafikiria kuingia Gaza kwa mashambulizi ya moja kwa moja.

Kundi la Hamas lilichukua udhibithi uongozi wa Gaza mwaka 2007.

Jeshi la Israel limezingira Gaza na kuzuia usafirishaji wa maji na mafuta.

Msemaji wa jeshi la Israel Hagari, amesema kwamba hakuna mshambuliaji wa Hamas ameingia Israel tangu walipotekeleza shambulizi la jumamosi.

Msemaji wa Hamas Abu Ubaida alisema Jumatatu kwamba wataua watu waliotekwa nyara kwa kila shambulizi Israel itatekeleza bila kutoa ilani, na kwamba watatangaza katika vyombo vya habari kila mtu watakayemuua.

Shambulizi la jumamosi, na majibu ya Israel, vinavuruga mpango wa diplomasia katika mashariki ya kati, wakati Israel ilikuwa katika hatua za kufikia makubaliano ya kuimarisha uhusiano na Saudi Arabia.

Nchi za magharibi zinaunga mkono Israel.

Maandamano yametokea katika miji ya kiarabu kuunga mkono Palestina.

Forum

XS
SM
MD
LG