Tume hiyo ya kuleta uthabiti ya Umoja wa Mataifa kwa Mali (MINUSMA) ilikuwepo nchini humo toka 2013, na kujiondoa kwake kunazusha hofu kwamba mapigano yatapamba moto baina ya jeshi la nchi hiyo na makundi ya wenye silaha.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema katika taarifa iliyochapishwa Jumapili kwamba MINUSMA imefikia ukomo wake katika muda uliokubaliwa wa Desemba 31.
Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa, ameipongeza tume hiyo kwa kuchukua jukumu muhimu la kuwalinda raia, na kusaidia mchakato wa amani ya Mali, ambayo imedhoofishwa na ghasia za makundi yenye msimamo mkali na migogoro mingine.
Forum