Raia wa Nigeria watapiga kura Februari 25 kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari ambaye ataachia madaraka baada ya mihula miwili madarakani inayoruhusiwa kikatiba.
Magavana wa majimbo na wabunge watachaguliwa wiki mbili baadaye.
Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika na lenye uchumi mkubwa sana, lina historia ndefu ya kasoro wakati wa uchaguzi, udanganyifu na ghasia.
Buhari, jenerali wa zamani wa jeshi mwenye umri wa miaka 79, ameahidi uchaguzi ulio huru na wa haki.
Ili kukuza haki, uaminifu na uwazi wa mchakato wa uchaguzi, Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC) ilianzisha mfumo wa kuidhinisha wapiga kura katika kura za mwaka 2015 na 2019.
Lakini mfumo huo uligubikwa na mapungufu.