Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 07:21

Tume ya uchaguzi Nigeria: vituo 240 havitatumika katika uchaguzi ujao

Wafuasi wa Mgombea Urais wa Chama cha Labour cha Nigeria, Peter Obi, wakiimba, wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Tafawa Balewa mjini Lagos Nigeria, Jumamosi, Februari 11, 2023.

Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Nigeria alisema Jumatatu kuwa vituo 240 vya kupigia kura havitatumika katika uchaguzi ujao, kwani hakuna aliyevichagua kutokana na ukosefu wa usalama katika maeneo hayo.

Vurugu za watu wanaojitenga na magenge ndio wasiwasi mkubwa kwa Wanigeria wanapopiga kura Februari 25 kwa ajili ya wabunge wapya na mrithi wa Rais Muhammadu Buhari.

Wapiga kura wapya wanapojiandikisha nchini Nigeria, wanaruhusiwa kuchagua kituo cha kupigia kura. Watu wengi huchagua eneo la karibu zaidi na wanapoishi kwa sababu idara za usalama hupunguza harakati za usafiri siku ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Mahmood Yakubu aliwaambia viongozi wa vyama vya siasa kwenye mkutano mjini Abuja kuwa tume hiyo imeongeza idadi ya vituo vya kupigia kura hadi 176,846 kutoka 119,973 miaka miwili iliyopita.

Hakuna hata mmoja wa wapiga kura zaidi ya milioni nane waliojiandikisha kati ya 2021 na 2022 aliyechagua kupiga kura katika vituo 240 kati ya vituo vipya, wakati wale ambao tayari wamejiandikisha hawakuonyesha nia ya kuhamishiwa hadi kwenye vituo vipya, alisema.

XS
SM
MD
LG