Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:50

Tume ya uchaguzi Kenya iko tayari


Wakenya wakisubiri kupiga kura katika shule ya msingi ya Westland, Nairobi wakati wa uchaguzi wa 2002.
Wakenya wakisubiri kupiga kura katika shule ya msingi ya Westland, Nairobi wakati wa uchaguzi wa 2002.

Akianza rasmi kazi zake Jumanne mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema wako tayari kwa upande wa mipango kwa uchaguzi mkuu wa 2012.

Akizungumza Jumanne wakati Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, ilipokuwa inakabidhiwa mamlaka rasmi na tume ya mpito, Bw. Ahmed Isaack Hassan amewahakikishia wa Kenya kwamba tume mpya ya uchaguzi iko tayari kuanda upigaji kura ikiwa ni Agosti au Disemba.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Bw. Hassan alikiri kwamba wangali na matatizo ya vifaa kwa wakati huu na kwamba mvutano juu ya kubadili tarehe ya uchaguzi huwenda ukachelewesha utaratibu na matayarisho.

Hiyo hiyo Jumanne Mahakama Kuu ya Kenya ilikata kuamua juu ya tarehe ya uchaguzi mkuu. Mahakimu wamependekeza kesi ifikishwe mbele ya mahakama ya katiba kwanza na mahakama ya juu kabla ya kufika mbele yao.

Bw Hassan anasema jukumu kuu lao kwa wakati huu ni kukamilisha kuchora mipaka ya wilaya za uchaguzi, na kuanza zowezi la kuwandikisha wapigaji kura ambao anatarajia kufikia watu milioni 20.

XS
SM
MD
LG