Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:21

Tume: Watanzania pigeni kura kwa amani


Mwenyekiti wa tume ya taifa uchaguzi Jaji Lewis Makame (kulia) akimkabidhi fomu mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha TLP Mutamwega Mugahywa.
Mwenyekiti wa tume ya taifa uchaguzi Jaji Lewis Makame (kulia) akimkabidhi fomu mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha TLP Mutamwega Mugahywa.

Tume ya taifa ya uchaguzi na viongozi wa dini wawasihi wapiga kura kuwa watulivu

Ikiwa zimebakia saa chache kabla ya watanzania kushiriki zoezi muhimu la uchaguzi mkuu kumchagua rais, wabunge na madiwani tume ya taifa ya uchaguzi imewasihi wapiga kura kushiriki zoezi hilo kwa amani na utulivu .

Mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw.Rajabu Kiravu amewasihi wapiga kura kutokaa katika maeneo ya kupigia kura na wakimaliza kupiga kura waende zao ili kuondoa hofu na wasi wasi kwa wale ambao bado hawajapiga kura.

Na kuhusu suala la wale ambao majina yao hayaonekani kwenye daftari la wapiga kura hata kama wana kadi, bwana Kiravu anasema hawaturuhusiwa kupiga kura na kwamba ni wajibu wa wapiga kura kuhakikisha majina yao yapo kwenye daftari hilo.

Nao viongozi wa dini kutoka jumuiya za kikristo na kiislam wamekutana na viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31.

Viongozi hao ni kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar , Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Jumuiya ya kikiristo Tanzania (CCT) na baraza la waislam Tanzania Bakwata . Kwa pamoja, wameomba viongozi wa kisiasa wawe na ustahimilivu na kuhakikisha baada ya uchaguzi nchi inabaki na amani.

XS
SM
MD
LG