Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:29

Utafiti wazuia Truvada kwa wanawake wenye HIV


Kidonge cha Truvada kilichobuniwa kuzuia maambukizo ya HIV kinatengenezwa na kampuni ya Gilead Science iliyopo California nchini Marekani.

Wafuatiliaji huru walishauri kusitishwa kwa jaribio la Truvada, baada ya kuhitimisha kwamba utafiti una wasi wasi mkubwa wa kutokuwa na matokeo yenye matumaini.

Watafiti wa madawa wanazuia jaribio la kidonge kimoja kilichobuniwa kuzuia maambukizo ya HIV kwa wanawake wa kiafrika kwa sababu kidonge hicho hakifanyi kazi vizuri.

Jaribio hilo linaloendeshwa na kitengo cha kimataifa cha afya ya jamii-FHI chenye makao yake hapa nchini Marekani, kinasema wafuatiliaji huru walishauri kusitishwa kwa jaribio la kidonge cha Truvada, baada ya kuhitimisha kwamba utafiti una wasi wasi mkubwa wa kutokuwa na matokeo yenye matumaini.

Watafiti kutoka kundi hilo lisilo la kiserikali walisema wiki hii kuwa wameshangazwa na kusikitishwa na utafiti wao kutokuwa na uwezo wa kuthibitisha kama tiba hiyo ya dawa ya kunywa inafanya kazi kuzuia maambukizo kwa wanawake wenye HIV, katika nchi za Kenya, Afrika Kusini na Tanzania.

Watafiti hao walikubaliana kusitisha majaribio yaliyowahusisha wanawake takriban 2,000 kutoka nchi hizi tatu katika miezi michache ijayo.

Kitengo cha FHI kilisema tiba kama hiyo itolewayo kwa njia ya kunywa ijulikanayo Pre-exposure Prophylaxis(PrEP) ilionyesha mafanikio kwa wanaume mashoga katika utafiti uliofanywa mwaka jana, hasa kwa kupunguza hatari zao za kuambukizwa virusi ambavyo vinasababisha ukimwi.

Watafiti wanasema sababu mojawapo ya kuwepo matokeo mabaya katika utafiti wa hivi karibuni ni kwamba wanawake ambao walishiriki huwenda hawakuwa makini katika utumiaji wa vidonge hivyo. Watafiti wanasema uchambuzi zaidi unahitajika kuona nini hakikuwa sahihi katika utafiti huo.

XS
SM
MD
LG