Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:27

Trump aandaa mpango wa kuzuia wahamiaji kutoka nchi zenye waislamu wengi


Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump.

Trump sasa ana mpango wa kutoa amri nyingine kuzuia watu wanaokuja kutoka nchi zenye waislamu wengi.

Rais Donald Trump ametoa amri za kiutendaji zinazotaka kujengwa ukuta kati ya mpaka wa Marekani na Mexico na kushinikiza kuzuia watu wanaohamia nchini kinyume cha sheria.

"Ni nchi zenye ugaidi wa ajabu, na ni nchi ambazo watu wake watakuja hapa nchini na kutuletea matatizo makubwa,” Trump amesema katika mahojiano yake Jumatano na shirika la habari la ABC.

Wale ambao wana uzoefu na rasimu za amri kama hizi tunaweza kusema itahusisha angalau upigaji marufuku kuingia nchini wa siku 30 kwa mtu yeyote anayetokea Iraq, Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen.

Wakati wa kampeni yake, Trump mwanzoni alipendekeza kupigwa marufuku waislamu wote kuingia Marekani, na baadae akabadilisha na sasa italenga nchi zenye ugaidi.

Usaili mzito utawakabili baadhi ya mataifa

Katika mahojiano alipoulizwa kuhusu nchi kama vile Afghanistan, Pakistan na Saudi Arabia ambazo haziko kwenye orodha ya zile zilizopigwa marufuku, alisema watu kutoka nchi hizo zilizokuwa hazijaorodheshwa watakabiliwa na usaili mzito.” Pia katazo hilo linaweza lisiwaguse wananchi ambao katika nchi zao wao ni wachache na wanakabiliwa na unyanyasaji.

Agizo hilo pia litaweka sitisho la miezi minne kwa wakimbizi wote wanaotaka kuja Marekani.

Azikosoa nchi za Ulaya

Trump amezikosoa nchi za Ulaya kwa uamuzi wao wa kuchukua maelfu ya watu ambao wamekimbia nchi zao, wengi kati yao ni kwa sababu ya vita, ugaidi na machafuko ya kisiasa katika nchi hizo. Amesema lakini baadhi yao wanakuja na “nia mbaya” wakiwemo wanachama wa kundi la wanamgambo la Islamic State

“Mimi nitakuwa ni rais wa nchi yenye amani,” Trump ameiambia ABC.

Pia amerejea kusisitiza kuwekwa maeneo salama nchini Syria. Fikra hii ni kwa sababu ya kuwawezesha watu wanaokimbia kutoka sehemu mbalimbali za Syria kuweza kwenda katika maeneo hayo badala ya kutafuta hifadhi nje ya nchi zao. Pia itawezesha kuongeza uwepo wa majeshi ya Marekani ilikuwalinda.

XS
SM
MD
LG