Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 19:06

Trump asisitiza Mexico italipia ujenzi wa ukuta


Trump akizungumza kwenye mkutano wa kampeni huko Arizona.

Mgombea urais kwa chama cha republikan hapa Marekani Donald Trump Jumatano usiku alitoa hotuba akieleza sera zake kuhusu uhamiaji akihimiza kuimarisha usalama mipakani na kuhakikisha wanaoingia Marekani wanaiheshimu.

Trump alitoa hotuba hiyo kwenye jimbo la Arizona wakati akitumia maneno mazito kuliko alivyofanya saa chache kabla alipokuwa nchini Mexico wakati wa kile kilichotajwa kuwa ni mkutano muhimu na Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto.

Trump aliendelea kushikilia msimamo wake wa kujenga ukuta kwenye mpaka wa Mexico huku akisema kuwa walizungumzia swala hilo na Rais wa Mexico ingawa Rais huyo alisema wazi kuwa nchi yake haitagharamia ujenzi wa ukuta huo.

Mwenyekiti wa kampeni ya Clinton John Podesta amesema Trump amejikaba mwenyewe kwa kutokuzungumzia suala hilo kwa ukamilifu na rais Pena Nieto.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG