Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:47

Trump akubali uteuzi wake kama mgombea kiti cha rais wa chama cha Republican


Mgombea urais wa chama cha Repablikan Donald Trump akikubali uteuzi Alhamisi usiku.
Mgombea urais wa chama cha Repablikan Donald Trump akikubali uteuzi Alhamisi usiku.

Migawanyiko badala ya umoja ni jambo ambalo lilishuhudiwa katika siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa chama cha Repablikan wakati mgombea urais wake Donald Trump alipokua akijiandaa kukubali uteuzi na kuanza rasmi kampeni zake dhidi ya mgombea mtarajiwa wa chama cha Demokrat na aliekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton.

Swala la mgawanyiko lilidhihirika usiku wa Jumatano pale Seneta wa Texas Ted Cruz alipomlaumu Trump na pia Alhamisi pale alipowaambia wajumbe kutoka Texas kuwa hatampigia Clinton kura lakini pia hakusema iwapo atampigia Trump wakati wa uchaguzi mkuu. Cruz alisema kuwa hana mazoea ya kuunga mkono watu wanaomuingilia mke wake. Wakati wa kampeni za awali,Trump alimshambulia mke wa Cruz, Heidi pamoja na baba yake Rafael.

Wakati huo huo miongoni mwa waliozungumza kwenye mkutano huo Alhamisi usiku ni mwanawe Trump, Ivanaka Trump ambae alisema kuwa baba yake anafaa kuongoza Marekani kutokana na ushahidi wa fanaka za biashara zake kote ulimwenguni, huku mgombea Trump akikubali uteuzi kwake na kusema kuwa atamaliza ghasia ambazo zimeendelea kushuhudiwa kwenye barabara za Marekani. Amesema serikali yake itazingaia swala la usalama.

XS
SM
MD
LG