Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:33

Trump kutangaza mgombea mwenza Ijumaa


Kutoka kushoto spika wa zamani Newt Gingrich, New Jersey Governor Chris Christie na Gavana wa Indiana Mike Pence.
Kutoka kushoto spika wa zamani Newt Gingrich, New Jersey Governor Chris Christie na Gavana wa Indiana Mike Pence.

Mgombea mtarajiwa wa chama cha Republikan Donald Trump anaendelea kupunguza watu anaotarajiwa kuchagua mgombea mwenza wa urais na anapanga kutoa tangazo lake Ijumaa.

Trump amesema katika mtandao wake wa Tweeter kwamba atatangaza saa 5 asubuhi Ijumaa katika jimbo la New York.

Kati ya wanaotarajiwa kupewa nafasi ni pamoja na Gavana wa Indiana Mike Pence ambaye alikuwa nae katika hafa ya uchangishaji fedha jumanne , spika wa zamani wa bunge la Marekani Newt Gingrich , na Gavana wa new Jersey Chris Christie .

Christie aliwahi kuwa mgombea wa chama cha republican na mpinzani wa Donald Trump katika uchaguzi wa awali ila aliamua kumuunga mkono mapema Trump baada ya kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

XS
SM
MD
LG