Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:44

Trump kusikiliza kero za wanafunzi, wazazi, waalimu Marekani


Rais Donald Trump na mkewe Melania na Dkt Igor Nichiporenko walipotembelea hospitali ya Broward ambako wanafunzi waliojeruhiwa katika shambulizi la bunduki katika shule ya Marjory Stoneman Douglas huko Parkland, Florida wakipatiwa matibabu.

Baada ya kupendekeza katazo la aina zote za vifaa ambavyo vinaweza kutengeneza silaha ambazo ni hatari sana na kutoa wito kuwepo uchunguzi wa maisha ya watu wote wanaonunua silaha, Rais wa Marekani Donald Trump anafanya kikao “kusikiliza maoni” juu ya silaha hizo Jumatano.

Kikao hicho kinafanyika huko ikulu ya White House na kitahudhuriwa na wanafunzi, wazazi na walimu ambao wamekuwa ni wahanga wa mauaji ya nchini Marekani.

Kati ya wale wanategemewa kuhudhuria mkutano huo ni wanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas huko Parkland, Florida ambapo mwanafunzi wa zamani Jumatano iliopita aliwaua watu 17.

Zaidi ya wanafunzi 100 wa shule hiyo pia watakusanyika Jumatano huko baraza la wawakilishi la Florida kutoa wito kuwepo kwa marekebisho ya udhibiti wa silaha.

Trump Jumanne ameyaita mauaji hayo ya kutumia silaha ni “mauaji ya kishetani.”

Rais akitoa maelezo yake ya kina kwa mara ya kwanza tangu mauaji ya Florida yatokee, alitangaza kuwa “usalama shuleni ni kipaumbele cha juu kabisa katika uongozi wake,” akiongeza kuwa atakuna na magavana wa jimbo wiki ijayo kujadili suala hilo.

XS
SM
MD
LG