Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 12:16

Trump amzungumzia Saddam Hussein


Saddam Hussein

Ni karibu miaka kumi sasa tangu kiongozi wa Iraq, Saddam Hussein, alipouwawa baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Jumanne, Hussein lilikuwa jina lililovuma sana kwenye mtandao wa Twitter baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Repablikan hapa Marekani, Donald Trump, kusifu uongozi wa Saddam Hussein.

Trump ameshawahi kutoa matamshi sawa na hayo hasa 2014 alipoandika kwenye Twitter kwamba Iraq sasa ni hatari kuliko ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Saddam Hussein.

Trump amesema kuwa aliekuwa Rais wa Marekani, George Bush, pamoja na Rais Barack Obama wanahitaji kuomba msamaha kwa kuamuru vita vya Iraq.

XS
SM
MD
LG