Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 20:43

Mueller kuchunguza iwapo Trump alivunja sheria


Mchunguzi maalum Robert Mueller
Mchunguzi maalum Robert Mueller

Mwendesha mashtaka maalum anayechunguza tuhuma za Russia kuingilia kati uchaguzi wa Marekani ataangalia kama Rais Donald Trump alizuia sheria kufuata mkondo wake.

Uchunguzi huo unaoangalia iwapo Russia ilihusika kwa njia isiyo halali kuvuruga uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana na uwezekano wa kusaidia kampeni ya rais Donald trump umepanua wigo kuangalia kama rais aliingilia kati sheria.

Hayo yamebainika jana jioni katika makala zilizochapishwa kwenye magezeti ya Washington Post, New York Times na jarida laWall Street Journal kulingana na maelezo ya watu ambao wanafahamu kuhusu uchunguzi huo.

Magazeti na jarida yamesema kuwa mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller anapanga kuwahoji Mkurugenzi wa Ujasusi wa kitaifa, Dan Coats, mkuu wa usalama wa taifa, Michael Rogers na aliyekuwa naibu wa mkuu wa shirika hilo, Richerd Ledgett.

Mueller anachunguza uwezekano wa kuhusika kwa njia yoyote, kwa timu ya kampeni ya Trump, kwenye sakata ambapo Russia inatuhumiwa kuingilia uchaguzi huo wa mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kuchunguza iwapo kulikuwa na pesa zilizotumika kwenye shughuli hizo, kwa njia isiyo halali.

Washington Post imeripoti kwamba awamu hiyo ya kuzuia haki kutendeka, ilianza pale Rais Trump alipomwachisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya FBI, James Comey.

XS
SM
MD
LG