Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:32

Wamarekani watamchagua rais mpya Novemba 8


Mgombea urais wa Republikan Donald Trump na mgombea urais wa Demokratik Hillary Clinton.
Mgombea urais wa Republikan Donald Trump na mgombea urais wa Demokratik Hillary Clinton.

Wamarekani watamchagua rais mpya Novemba 8, wakati masuala kama vile uchumi na sera za mambo ya nje yatakuwa ni muhimu, ukusanyaji maoni unaashiria wapiga kura wengi huenda wakafanya maamuzi yao kulingana na jinsi wanavyoangalia sifa binafsi za wagombea wawili wa juu, Mdemocrat Hillary Clinton na Mrepublican Donald Trump.

Masuala ya tabia yametawala kampeni za uchaguzi wa mwaka 2016 kuanzia mwanzo, na inaonekana hayaondoki katika siku za mwisho za kampeni wakati Clinton na Trump kila mmoja bado analenga kuzungumzia makosa ya mwenzake.

Kuanzishwa kwa uchunguzi mpya na shirika la upelelezi la marekani (FBI) kuhusiana na Clinton kutumia tarakilishi binafsi kwa barua pepe wakati akiwa waziri wa mambo ya nje yamesukuma juu kwa mara nyingine tena suala la uaminifu.

Trump hakupoteza muda katika kuzungumzia maendeleo hayo katika mikutano yake ya kampeni, ikiwa pamoja na ule alioufanya Phoenix, Arizona.

“Hii ni kadhia kubwa sana ya kisiasa tangu ile ya Watergate, na ni matumaini ya kila mmoja kwamba haki, hatimaye, itapatika kwa njia nzuri, “ amesema Trump.

​
XS
SM
MD
LG