Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 04:09

Trump kupewa muhtasari kamaili wa uhalifu wa Russia


Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Upelelezi, James Clapper.
Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Upelelezi, James Clapper.

Mkuu wa idara ya usalama wa taifa, Mike Rogers anasma anafikiri kuna tofauti kati ya kuwa na wasi wasi wa tahadhari na kufanya kejeli.

Rais-mteule wa Marekani, Donald Trump, ambaye ameukataa msimamo wa idara za upelelezi za Marekani kwamba Russia ilihusika na uhalifu wa mitandao katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa urais, atapokea muhtasari kamili wa shutuma hizo kutoka kwa viongozi hao Ijumaa.

Katika hali ambayo haikutarajiwa kwa rais mteule, Trump amekuwa akizshutumu idara hizo, lakini Alhamisi alilegeza kamba kwa namna fulani pale alipotuma ujumbe wa Twitter kwamba yeye ni “mshabiki mkubwa” wa jumuiya ya wapelelezi.

Upo ushahidi Russia kuhusika
Alhamisi wakuu wa vyombo vya upelelezi walitoa ushahidi wakisema kwamba hakuna shaka kwamba Russia iliingilia kati uchaguzi wa rais Novemba lakini wakasema hawawezi kujua kama hilo lilimsaidia Trump kushinda.

“Russia ina historia ndefu ya kuingilia uchaguzi wa nchi nyingine, nchini kwao na za watu wengine,” mkurugenzi wa upelelezi wa taifa, James Clapper ameiambia kamati ya seneti ya shughuli za kijeshi.

“Lakini hatujawahi kukabiliwa na aina ya kampeni chafu iliyo ingiliana moja kwa moja na machakato wa uchaguzi kama tulivyoona katika suala hili.

Clapper amewaambia maseneta kuwa Russia ilitumia mbinu mchanganyiko katika kampeni yake ya sio tu kujipenyeza katika mitandao na kuvujisha barua pepe za chama cha Demokratik, lakini pia kueneza propaganda, upotoshaji wa taarifa na habari feki.”

Clapper amesema hana uhakika kama uvujishaji wa taarifa hizo nyeti uliwaghilibu wapiga kura kufanya maamuzi katika uchaguzi wa Novemba 8. Lakini alisema Russia haikuingilia katika kuhesabu kura au matokeo ya uchaguzi.
Maafisa wa ngazi ya juu wahusishwa

Clapper aliungana na mkuu wa shirika la usalama wa taifa, Mike Rogers na maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani Alhamisi kusema isingewezekana Moscow kuingilia uchaguzi bila ya ruhusa ya moja kwa moja kutoka kwa “ maafisa wa ngazi ya juu kabisa wa Russia.”

Hata hivyo Clapper ametoa taarifa za kipelelezi kwa uchache dhidi ya Russia Alhamisi, akisema kutoa taarifa kamili kwa umma kunaweza kuteteresha shughuli za kipelelezi.

“Tumewekeza mabilioni ya fedha na tumewaweka watu wetu katika hatari kubwa juu ya maisha yao katika ukusanyaji wa taarifa hizi,” alisema Clapper. Aliwaambia maseneta kwamba taarifa zilizokuwa hazihatarishi usalama wa nchi juu ya kadhia hii ya ripoti hii nyeti zitatolewa wiki ijayo.

“Nafikiri umma unatakiwa kujua kadiri itavyowezekana juu ya suala hili, kwa hivyo tutakuwa tayari kuwapa taarifa kila itapowezekana. Lakini kuna baadhi ya mambo nyeti na watoa habari walioko hatarini na taratibu kufuatwa,” Clapper alisema.

Wademokrat wengi wanaamini kuwa uhalifu wa Russia wa mitandao ulidhamiria hasa kumsaidia Trump kushinda kwenda Ikulu ya White House dhidi ya mpinzani wake Hillary Clinton. Baadhi ya wawakilishi wa Republikan katika bunge la Marekani wanadai kuwa uchafuzi wa aina yeyote unao kikusudia chama chochote cha kisiasa ni kosa la jinai.

Trump avutiwa na Putin

Trump hata hivyo ameweka wazi kuvutiwa kwake na rais wa Russia, Vladimir Putin, ambaye anasema kwamba ana mashaka makubwa juu ya Russia kujihusisha na uhalifu wa mitandao na hakuonyesha kuridhishwa na idara za upelelezi za Marekani.

“Nafikiri kuna tofauti muhimu hapa kati ya wasiwasi wa tahadhari ambao watunga sheria akiwemo rais mwenyewe akiwa namba moja wanatakiwa kuwa nao kwenye masuala ya kipelelezi," Clapper amesema alipoulizwa kuhusu Trump. “Lakini nafikiri kuna tofauti kati ya kuwa na wasiwasi wa tahadhari na kufanya kejeli.”

XS
SM
MD
LG