Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 09:13

Katika kitabu kipya, Bannon amlaumu Trump kuhusu Russia


Rais Trump, kushoto, na msaidizi wake wa zamani Steve Bannon.

Msaidizi wa zamani wa Rais Trump, Steve Bannon anasema ilikuwa kitendo cha "uhaini" na "kinyume cha uzalendo" kwa mtoto wa Rais na meneja wa kampeni yake kukutana na Warussi katikati ya kampeni ya mwaka 2016, kulingana na maelezo katika kitabu kipya.

Katika kitabu kipya kinachotazamiwa kutolewa karibuni Bannon anamlamu Donald Trump Jr., mkwe wa Rais Trump Jared Kushner, ambaye sasa ni msaidizi katika Ikulu, na meneja wa kampeni wakati ule Paul Manafort kwa kuhudhuria mkutano June 2016 na Warussi katika jengo la Trump Tower mjini New York.

Mkutano huo uliandaliwa na Trump mdogo baada ya kuambiwa na mjumbe mmoja wa Ulaya kwamba Warussia wana habari ambayo inaweza kumtia matatani Hillary Clinton, mgombea urais kutoka chama cha Democratic.

Trump mdogo alisema "angependa" kupata habari inayoweza kumharibia Clinton, ingawa alisema baadaye mwanasheria wa Kirussi waliyekutana naye hakuwa na habari yoyote ya namna hiyo.

"Watu watatu wa ngazi za juu katika kampeni walidhani ni wazo zuri kukutana na serikali ya nje ndani ya Trump Tower katika chumba cha mkutano, ghorofa ya 25 - bila wanasheria, " Bannon anakaririwa katika kitabu hicho kipya cha Michael Wolff, kinachoitwa "Fire and Fury: Inside the Trump White House."

"Hata kama unadhani (hatua) hiyo haikuwa uhaini, au kinyume na uzalendo ......ulitakiwa kuitaarifu FBI haraka," Bannon alisema.

Bannon alikuwa mtendaji mkuu wa kampeni ya Trump katika miezi mitatu ya mwisho kabla ya uchaguzi wa Novemba 2016, na baadaye alikuwa kiongozi wa mikakati katika Ikulu ya Trump kwa miezi saba ya utawala wake kabla kuondoka na kurudi kufanya kazi katika mtandao wa habari wa Breitbart News.

White House imekanusha matamshi ya Bannon huku vyombo vya habari Marekani vikiripoti kuwa Rais Trump amemwita Bannon kama mtu ambaye hakuwa na ushawishi wowote katika Ikulu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG