Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:11

Trump azindua meli ya kivita ya USS Gerald Ford


 USS Gerald R. Ford, meli ya kivita iliyozinduliwa na rais Donald Trump katika mki wa Norfolk, Virginia.
USS Gerald R. Ford, meli ya kivita iliyozinduliwa na rais Donald Trump katika mki wa Norfolk, Virginia.

Rais Donald Trump siku ya Jumamosi alizindua meli ya kivita iitwayo USSR Gerald R Ford, ambayo inatumia nguvu za kinyuklia na iliyogharimu karibu dola bilioni 13 kwa ujenzi wake kukamilika.

Uzinduzi huo ulifanyika katika mji wa Norfolk, Jimbo la Virginia, Marekani.

Trump alisema kuwa maadui wa Marekani watakuwa wakitetemeka watakapoinona meli hiyo ikikaribia.

Ujenzi wa meli hiyo, ambayo pia ni ya kubeba ndege za kijeshi, ulianza mnamo mwaka wa 2009 na ulitarajiwa kukamilika mnamo mwaka wa 2015 kwa gharama ya dola bilioni 10.5.

Hata hivyo, ujenzi wake ulichukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa kuliko ilivyokadiriwa. Jeshi la majini lilisema kuwa kucheleweshwa huko, na ongezeko hilo la gharama, ni kutokana na mahitaji ya teknolojia ya kisasa ambayo imetumika kujenga meli hiyo.

USS Ford, imepewa jina la rais wa 38 wa Marekani, ambaye alihudumu kama Luteni kamanda wa jeshi la wanamaji wakati wa vita vya pili vya dunia. Alikuwa rais kati yam waka wa 1974 na 1977.

XS
SM
MD
LG